Tuesday, April 5, 2016

Dr. Shein: Sitoteua Makamu wa Kwanza wa Rais toka Upinzani, hawakukidhi vigezo

Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la 9 la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM. 


Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ifipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

JIFUNZE NAMNA YA KUENDESHA BIASHARA YAKO HAPA KWA HUYU NDUGU.

KAMA UNA NDOTO YA  # KUJIJIRI  AU KUFANYA  # BIASHARA  USIOGOPE ILA JIFUNZE KIDOGO HAPA! Naitwa Andrea. Na nakutana na watu we...