Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa,kesho Desemba 14,2017
anatarajia kuwaongoza waombolezaji kwenye shughuli ya kuaga miili ya wanajeshi
14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliouawa wakati
wakitekeleza majukumu ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo,DRC
Taarifa ya
Kurugenzi ya Mawasiliano Makao Makuu ya JWTZ imeeleza kuwa shughuli ya kuaga
miili hiyo itafanyika katika viwanja vya makao makuu ya JWTZ yaliyopo Upanga
jijini Dar es salaam
Taarifa hiyo
imeeleza kuwa shughuli ya kuaga itaanza mapema asubuhi na kuhudhuriwa pia na
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo na wakuu wengine wa vyombo vya ulinzi
na usalama
Aidha
imeongeza kuwa baada ya kukamilika kwa shughuli ya kuaga,miili hiyo
itasafirishwa kwenda makwao kwa ajili ya mazishi
Wanajeshi hao
14 waliuawa baada ya kushambuliwa na waasi wakati wakitekeleza jukumu la
kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo chini ya vikosi vya Umoja
wa Mataifa ambapo katika shambulio hilo,wanajeshi wengine 44 walijeruhiwa na
wawili wengine hawajulikani walipo