Namna unavyoweza kumsaidia mtoto mwenye mafua.
Punguza speed ya kutokwa na makamasi kwanza.
Mtoto kuwa na mafua huwa ni kitu cha kawaida, na kugundua utaanza kuona anatokwa na makamasi muda wote na hizi dalili unaweza kuziona zinadumu kwa muda wa wiki moja au mbili basi ukiona hivyo basi ujue mtoto wako ana mafua.
Makamasi kwanza yataanza kuwa ya kawaida mepesi tu alafu baadae yataanza kuwa ya njano.
Jinsi ya kupunguza spidi ya kutokwa na makamasi jaribu kumpa maji yenye chumvi huwa yanasaidia kupunguza speed ya kutokwa na makamasi kwa wingi.
Msafishe pua yake.
Hii ni nzuri kama ukimuogesha mtoto wako kila mara pale anapokuwa amechafuka. Mpikie supu yoyote iwe ya ngombe au ya kuku hii nayo huwa inasaidia sana. Kama ukiona mtoto wako anatakiwa kumuona daktari na kupata dawa basi muone daktariā¦.sio kwenda kuchukua dawa yoyote tu ukampa. Nenda hospitali kwanza wakupe dawa.
Gundua ni muda gani kikohozi chake na mafua yanahitaji msaada zaidi.
Kukohoa huwa ni kawaida kama kuna kitu kimekukaba kwenye koo. Kukohoa huwa kunaisha baada ya muda, ila sasa kama kukohoa huko kunamfanya mtoto wako asilale usiku, anapa tabu kupumua vizuri au kinamsumbua hapo sasa inabidi uongeze jitihada za kumhudumia. Kama mtoto wako ana umri wa kuanzia mwaka mmoja kijiko kimoja cha chai cha asali kinaweza kumsaidia aache kukohoa na kama ukiona bado hali inaendelea basi mpeleke hospitali wakamuangalie vizuri.
Kupiga chafya
Jaribu kusikiliza jinsi mtoto wako anavyopumua ili ujue ni jinsi gani unaweza kumsaidia. Kupiga chafya mara kwa mara ni dalili pia ya kuonesha kuwa mtoto wako ana mafua, vile vile kutoa mlio kwa mbaali kama anapiga mluzi, hii utamuona tuu mtoto wako anakua hayuko katika hali ya kawaida hatulii anajitingisha tingisha. Hii inaweza kuwa ni dalili ya asthma au mafua, so ukiona mtoto wako anapata tabu ya kupumua, anashindwa kuongea, au anapumua kwa haraka sana kuliko kawaida basi kimbia hospitali mara moja.
Mhudumie muwasho na maumivu mengine.
Yaani mtoto akipatwa na mafua kuna uwezekano wa yeye kupatwa na maumivu mengine kama kichwa kuuma, mwili kuwashwa. Mafua yanaweza kabisa kumfanya mtoto wako ajisikie mwili mzima unauma.
Ili kumsaidia mtoto wako na hili tatizo muulize daktari wako kuhusu dozi ambayo anatakiwa kupewa kulingana na umri wa mtoto wako. Usimpe mtoto wako aspirini hata aspirini za watoto labda daktari wako awe amekuruhusu.
Msaidie mtoto wako apumzike.
Kama mtoto wako ana umri mkubwa wa kuanzia miaka mitano mpaka saba anaweza kuwa anaumwa na bado anataka kwenda kucheza haoni kama anahitaji kutulia. Sasa iko hivi, mtoto wako anaweza kuwa anachoka kwa sababu mwili wake unafanya kazi kubwa sana kujaribu kipigana na ugonjwa unaomsumbua.Sasa kwa kumsaidia atulie ndani apumzike ni njia nzuri ya kuharakisha awahi kupona. Mwambie akae ndani kama ni kusoma vitabu, au kuangalia vipindi vizuri vya watoto kenye TV, hii itamfanya atulie na kumpumzika wakati anauguza ugonjwa wake. Ila sasa ukimuachia akaenda nje kucheza na bado anaumwa na anakunywa dawa, hapo ndipo utaanza kujiuliza kwa nini mtoto haponi na wakati anakunywa dawa kila siku.
Muone Daktari
Hapa ndio huwa kuna utata kwa wazazi wengi. Kwa kuwa sisi tumezoea tukiumwa tunaenda pharmacy na kuchukua dawa tunakunywa maisha yanaendelea. Ila hii tabia ni kitu tofauti kabisa kwa upande wa watoto. Watoto wao wanahitaji kupimwa kwanza ujue ni nini kinamsibu hasa watoto wenye umri wa chini ya miaka 7. Ukimpa mtoto dawa ambazo sio za umri wake huwa zinakuja kuleta madhara baadae.
Haya sasa kama unaona unashindwa kwenda kwa daktari kwanza basi kuwa makini na dawa unazochukua. Hakikisha unachukua dawa ambazo zinaenda kutibu ugonjwa ambao mtoto wako anaumwa, na usichanganye dawa ambazo utengenezaji wake unaendana au unalingana, ndio maana inashauriwa ni bora uende tu kwa daktari upate dawa sahihi maaana unaweza ukamchanganyia madawa hapo galaxy ikaja kuwa balaa.
Pia mtoto alale sehemu safi,mashuka masafi,foronya za mito zifuliwe kila siku.Chumba chake kiwe kisafi kisiwe na vumbi kifanyiwe usafi kila siku.
|