Tuesday, April 26, 2016

Maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano, Wafungwa waneemeka.





Rais Dk.John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa wote kwa kuwapunguzia 1/6 ya vifungo vyao huku wafungwa 3,551 wakifaidika na msamaha huu baada ya kupunguziwa 1/6 ambao kati yao 580 watachiliwa huru na 2,971 wanabaki gerezani wakitumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 42 ya muungano kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1)(d) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao utawahusu wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya ukimwi, kifua kikuu, na kansa ambao wako kwenye hatua za mwisho, wafungwa waliothibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa mkoa au wilaya.
Wengine ni wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao umri huo umethibishwa na jopo la waganga, wafungwa wakike walioingia na mimba gerezani na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya pamoja na wenye ulemavu wa mwili na akili ambao pia wamethibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa mkoa au wilaya.
Msamaha huo hautawahusu waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa ama kifungo cha maisha, makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya,uombaji na upokeaji rushwa, unyang’anyi kwa kutumia silaha, makosa ya kupatikana na silaha, risasi na milipuko isiyo halali.
Wengine ni wale wanaokabiliwa na makosa ya shambulio la aibu, ubakaji, kunajisi na kulawiti, wenye makosa ya kuwapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliotenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka 18 na kuendelea, wizi wa magari, pikipiki, wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao, waliowahi kupunguziwa kifungo na msamaha wa rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
Waliohukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, biashara ya binadamu, kukutwa na viungo vya binadamu pamoja na vitendo vya mashambulizi na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, usafirishaji wa nyara za serikali na ujangili,wizi/ubadhilifu wa fedha za serikali, kujaribu kutoroka wakiwa chini ya ulizi halali na wale walioingia gerezani baada ya tarehe 26/02/2016.

TCRA YAPATIKANA









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.
Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.
“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua  dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson MsigwaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULUDar es salaam

JIFUNZE NAMNA YA KUENDESHA BIASHARA YAKO HAPA KWA HUYU NDUGU.

KAMA UNA NDOTO YA  # KUJIJIRI  AU KUFANYA  # BIASHARA  USIOGOPE ILA JIFUNZE KIDOGO HAPA! Naitwa Andrea. Na nakutana na watu we...