Naitwa Andrea.
Na nakutana na watu wengi kila siku ambao wamechoka kuajiriwa na wanataka kufanya kitu cha kwao wenyewe. Na siyo mbaya.
Na nakutana na watu wengi kila siku ambao wamechoka kuajiriwa na wanataka kufanya kitu cha kwao wenyewe. Na siyo mbaya.
Lakini kama wewe pia una mpango wa kufanya biashara basi tambua mapema kabisa kuwa kuna biashara za aina mbili:
1. Moja ni biashara zinazoweza kukutengenezea pesa na
2. Mbili ni biashara zinazoweza kukufanikisha.
2. Mbili ni biashara zinazoweza kukufanikisha.
Changamoto ipo kwenye kuzitofautisha.
Watu wengi wamejikuta wanaanza biashara na hawapati mafanikio yoyote kibiashara sababu toka wanaanza hawakujua mafanikio kwenye biashara yanaletwa na nini.. wengi wanafikiri ukianzisha biashara yoyote ile halafu ukafanya kazi tu kwa bidii basi utafanikiwa!

Ukweli ni kwamba kufanya kazi kwa bidii tu haisaidii chochote kama unachofanya ni the WRONG BUSINESS. Hujawahi kuona mtu ameanza biashara mahali na ana bidii ya kufa mtu lakini hafanikiwi. See? Lazima kwanza ujue kama biashara unayotaka kufanya ina potential ya kukufanikisha.
Idadi ya watu inaongezeka nchini kwetu na duniani kila mwaka. Ulisikia Tanzania tulikuwa watu milioni 45 hivi miaka kadhaa iliyopita lakini sasa hivi ni zaidi ya milioni 52. Watu wameongezeka kweli kweli.
Hii inamaana wahitaji wa bidhaa (wateja) wanaongezeka..si ndiyo? Mfano watu wanaohitaji kula, kuvaa, kuoga, kusafiri, nk wameongezeka.
Lakini wafanyabiashara wengi wanahangaika kupata wateja! Swali la kujiuliza ni mbona population inaongezeka halafu huyu mfanyabishara anasema hakuna wateja wakati wenzake wanazidi kupata wateja wengi zaidi?
Tatizo ni kuwa watu wengi wanatamani sana kufanya biashara na wengi wao hukurupukia ulimwengu wa biashara bila MAARIFA sahihi #machache tu ya msingi ya biashara.
Ni muhimu ukawa na maarifa hayo machache ya msingi ili sasa ukiamua kufanya biashara angalau unakuwa siyo tu kuwa unawekeza hela zako kwa kuwa umeambiwa eti biashara fulani inalipa. Bila maarifa utaendelea kusema vyuma vimekaza wakati wenzako wanapata pesa kumbe hujui tu kuwa tatizo ni huna maarifa sahihi tena machache.
Kwa mfano kila "era" ya maisha ina biashara zake. Biashara za miaka ya 70, 80 na 90 ni tofauti sana na za zama hizi za miaka ya 2000+. Ndo maana Mark Zuckerberg alianzisha Facebook mwaka 2004 tu lakini leo ni tajiri namba 5 kwa utajiri duniani na kuna watu walianza mwaka 70 na hawajafika mbali. Simaanishi kudhalilisha chochote no najaribu tu kufafanua kitu. Unielewe. So why Zuckerberg amefika mbali hivyo kwa muda mfupi?
Sababu anaoperate katika biashara ya zama hizi. Angeamua kufungua saluni mwaka 2004 nayo ingekuwa biashara tu tena ni nzuri na marafiki huenda wangemsifia kuwa anajituma ni mchakarikaji nk lakini hakika asingekuwa alipo leo.
Kuna watu huniambia "Lakini kaka Andrea hakuna biashara isiyolipa bwana" Na mi huwajibu tu kuwa "Of course hakuna ila kuna tofauti ya #kukulipa na #kukufanikisha" Na huwa nawauliza "Wewe unataka biashara ya kukulipa tu au ya kukufanikisha?"
Malipo siyo ishu. Mshahara ni malipo pia lakini si rahisi yakakufanikisha kiuchumi. Na biashara ziko hivyo. Inabidi uwe tayari kujifunza kujua biashara ipi itanipa tu pesa na ipi itanifanikisha kiuchumi. Hushangai kwa nini HAKUNA tajiri mwenye duka au saluni nk. Kwani hawana mitaji ya kufungua maduka au saluni?
Jibu ni kuwa kama kulivyo na makazi ya maskini na ya matajiri, mavazi ya kimaskini na ya matajiri, magari ya kimaskini na ya kitajiri nk ndivyo kulivyo na biashara za #kimaskini na za #kitajiri. Tatizo siyo bidhaa. Mfano karanga. Diamond anatumia mfumo wa kitajiri. Karanga zinamfanikisha.
Hana duka na anauza kuliko wenye maduka. Wao wanapata tu pesa. Yeye anafanikiwa. Vitu hivi hutavifahamu kirahisi kama badala ya kujifunza vitu vya aina hii wewe utabakia kushabikia posts za watu wanaojadili vitu visivyo na faida yoyote kwako kibiashara. Tumia mitandao ya kijamii vizuri utashangaa jinsi utakavyopata maarifa makubwa sana ya kukufaa. Huwezi kusema unataka kuwa mfanyabiashara wakati muda mwingi unautumia kuangalia clip za umbea tu na vikatuni katuni. Delete hivyo vitu from your phone. Biashara ni kitu serious.
Be serious pia.