Showing posts with label News. Show all posts
Showing posts with label News. Show all posts

Friday, January 12, 2018

SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR ZAFANA

Rais wa Nzanzibar Dr Shein akiwasili katika sherehe za mapinduzi zilizofanyika leo 12/01/18

Rais wa Zanzibar akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za mapinduzi leo 12/01/2018

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika sherehe za mapinduzi 

Rais Magufuli , Mama Samia pamoja na waziri mkuu Kassim Majaliwa nao ni baadhi ya viongozi walio hudhuria sherehe hizo

Monday, December 25, 2017

HABARI KATIKA PICHA: CCM YA MOTO







Hii ilikua ni asubuhi ya siku ya tarehe 18/12/2017. Kabla ya mkutano wa CCM Dodoma

Thursday, December 14, 2017

TANZANIA YAOMBA UMOJA WA MATAIFA KUFUATILIA KWA KINA VIFO VYA WANAJESHI WETU


Tanzania imeutaka Umoja wa Mataifa UN kufanya uchunguzi wa kina na huru kuhusu chanzo cha tukio la shambulio la waasi wa kundi la ADF lililosababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliokuwa wakilinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC.
Akizungumza kwenye shughuli ya kuaga miili ya wanajeshi hao iliyofanyika katika viwanja vya makao makuu ya JWTZ Upanga,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kuchunguza tukio hilo na kwamba serikali ya Tanzania inaamini uchunguzi huo utaanza hivi karibuni
"Japo matukio kama haya hutegemewa na hutokea,lakini hatujawahi kupoteza wapiganaji wengi na kwa mpigo kama hivi”.Amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Hata hivyo Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani nchini DRC wasirudi nyuma au kukatishwa na tukio hilo badala yake amewaasa kuchukua tahadhari zaidi.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi amesema wanajeshi waliouawa ni mashujaa wa Taifa na kuondoka kwao kumeacha pengo kubwa katika Taifa.
Dkt. Mwinyi amesema “Kuondoka kwa wanajeshi hawa kusiturudishe nyuma katika majukumu yetu ya kazi bali iwe chachu ya utendaji kazi na kutoogopa chochote kilichopo mbele yetu”

Naye Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo amesema mbali na wanajeshi 14 waliouawa,kuna mwanajeshi mmoja hajulikani alipo na kwamba wanajeshi wengine 44 ambao ni majeruhi wa tukio hilo wanaendelea na matibabu katika miji ya Kampala, Kinshasa na Goma.
Viongozi wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Afrika Dkt Salim Ahmed Salim,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC Dkt. Stagomena Tax,Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa UN na viongozi wa vyama vya siasa,dini na taasisi mbalimbali



MBUNGE MWINGINE WA CHADEMA AJIUZULU

Breaking news

Wednesday, December 13, 2017

Waziri Mkuu Majaliwa kuongoza shughuli za kuaga miili ya wanajeshi 14 waliouawa DRC



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa,kesho Desemba 14,2017 anatarajia kuwaongoza waombolezaji kwenye shughuli ya kuaga miili ya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliouawa wakati wakitekeleza majukumu ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Makao Makuu ya JWTZ imeeleza kuwa shughuli ya kuaga miili hiyo itafanyika katika viwanja vya makao makuu ya JWTZ yaliyopo Upanga jijini Dar es salaam
Taarifa hiyo imeeleza kuwa shughuli ya kuaga itaanza mapema asubuhi na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo na wakuu wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama

Aidha imeongeza kuwa baada ya kukamilika kwa shughuli ya kuaga,miili hiyo itasafirishwa kwenda makwao kwa ajili ya mazishi
Wanajeshi hao 14 waliuawa baada ya kushambuliwa na waasi wakati wakitekeleza jukumu la kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo chini ya vikosi vya Umoja wa Mataifa ambapo katika shambulio hilo,wanajeshi wengine 44 walijeruhiwa na wawili wengine hawajulikani walipo


Tuesday, December 12, 2017

MWENYEKITI WA CCM DR. JOHN MAGUFULI, LEO AMEFUNGUA MKUTANO WA JUMUIYA YA WAZAZI


Rais John Magufuli akifungua mkutano mkuu wa tisa wa umoja wa wazazi Tanzania leo tarehe 12/12/2017 mjini Dodoma.

Tuesday, May 10, 2016

Raisi Mstaafu naye aenda kushangaa kigamboni.



Raisi mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mke wake walipotembelea daraja la kisasa la Mwalim Nyerere.

Monday, May 9, 2016

AGIZO LA MAKONDA (MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM) LAGONGA MWANBA.



AGIZO la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lagonga mwamba baada ya baada ya ombaomba hao kuonekana barabarani wakiomba kama ilivyokuwa kawaid yao.

Ikiwa Mkuu wa Mkoa huyo alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwaondoa Ombaomba wote wanaoomba barabarani ifikapo Aprili 18 mwaka huu.Ombaomb ambaye jina lake halikupatikana mara moja


























akiomba msaada kwa wasamalia wema katika barabara ya Bibititi jijini Dar es Salaam. Mremavu wa Mguu akionekana kwenye maungio ya... 

TAARIFA YA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) KUHUSU VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO KWA KUJITOLEA NA KUTAKA KUAJIRIWA NA SERIKALI




Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa Julai 10, 1963 na serikali kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana wa nchi hii na kuwapa malezi kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru.
Baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa JKT ni:
Kubadili fikra za vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya ukoloni kutegemea nchi nyingine kuleta maendeleo.
Kukusanya nguvu za vijana wote wa nchi hii na kuzielekeza kwa umoja wao kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya taifa.
Kuwafunza vijana kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa, ili kulinda uhuru wa Taifa lao.
Jeshi la Kujenga Taifa linaunganisha vijana bila kujali itikadi zao, dini, elimu, jinsia na mali ili kuwalea kuwa wazalendo kwa taifa lao na kupenda kuitumikia nchi yao.
Pamoja na dhana ya kufunzwa uzalendo, pia stadi mbalimbali za kazi hufundishwa kwa vijana hao ili waweze kujiajiri, pindi wamalizapo mkataba yao ya kujitolea kwa miaka miwili.
Serikali ilirejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa vijana wa kujitolea mwaka 2001, baada ya kusitishwa mwaka 1994.
Masharti ya Kujiunga na JKT kwa vijana wa Kujitolea
Kijana kabla ya kujiunga na JKT hutakiwa kuyajua masharti na kuzifahamu taratibu za kujiunga na kuelewa kuwa JKT halitoi ajira.
Moja ya kipengele cha masharti ya kujiunga na JKT kinasema kuwa ‘Kwa kipindi chote nitakachokua ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi’.
Kipengele hiki kinaainisha masharti ya makubaliano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa na kijana kabla ya kujiunga na kupatiwa mafunzo ya awali ya kijeshi.
Aidha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine mara kadhaa wamekuwa wakisisitiza kuwa, JKT halitoi ajira.
Lakini hivi karibuni wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge mwaka huu, umezuka mtindo wa makundi ya vijana waliopitia JKT katika Operesheni mbalimbali kuomba kuandamana kwenda Ikulu kudai ajira.
Madai yanayopingana na dhana ya JKT na kauli ya Mhe. Rais kuwa Jeshi la Kujenga Taifa haliajiri, bali vijana hujiunga kwa hiari kwa kujitolea na baada ya mkataba wa miaka miwili wanatakiwa kurejea walikotoka.
Aidha, Mhe. Rais Kikwete, amewahi kutoa agizo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, taasisi za Serikali na kuziomba zile zisizoza kiserikali kutoa ajira kwa vijana waliopata mafunzo ya JKT kulingana na sifa za kijana na nafasi zilizopo.
Takwimu zinaonesha kuwa tangu kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT mwaka 2001 hadi mwaka jana, jumla ya vijana 104,594 wamejiunga na JKT wakiwemo wavulana 76,832 na wasichana 27,762.
Katika kipindi hicho, jumla ya operesheni 13 katika mafunzo ya JKT zimefanyika, Operesheni hizo ni pamoja na Operesheni Mkapa mwaka 2001, Miaka 40 ya JKT mwaka 2002, Utandawazi mwaka 2004 na Operesheni Jiajiri mwaka 2005.
Zingine ni pamoja na Kasi Mpya mwaka 2006, Maisha Bora mwaka 2007, Uadilifu mwaka 2008, Kilimo Kwanza mwaka 2009 na Operesheni Uzalendo mwaka (2010), Miaka 50 ya Uhuru (2011), Sensa mwaka 2012, Miaka 50 ya JKT (2013) na Miaka 50 ya Muungano (2014).
Vijana wa Kujitolea walioajiriwaTangu mwaka 2003 hadi 2014 jumla ya vijana 24,708 wameajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama ambapo vijana 21,977 wakiwemo wavulana 17,307 na wasichana 4,670 wameajiriwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jeshi la Polisi vijana 3,965 wavulana wakiwa 2,943 na wasichana 1,022, Magereza vijana 2,139 wavulana 2,044 na wasichana ni 95, Zimamoto vijana 100 wavulana wakiwa ni 78 na wasichana ni 22 na taasisi zingine vijana 592 Vijana 1,622 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali kama TANAPA, GEITA GOLD MINE, BANDARI na AFRICAN GOLD MINE.
Ni vema vijana hao wakatambua kuwa tatizo la ajira sio kwao peke yao, ni tatizo la ulimwengu mzima Tanzania ikiwemo, wanashauriwa kutumia stadi za kazi kujiajiri wenyewe.
Aidha, vijana hao watambue kuwa walikula kiapo cha UTII, wakati wa kuhitimu mafunzo ya JKT, hivyo suala la kuandamana ni kinyume cha kiapo chao. Vijana hao walitumikia Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni za nyuma na kumaliza mkataba wa miaka miwili. Shinikizo lao la kulazimisha ajira kwa kuandamana ni kinyume cha sheria za nchi.
Kwa maelezo ya hapo juu utaona kuwa Jeshi la Kujenga Taifa, halina dhamana ya kuajiri bali kufunza vijana wa taifa hili umoja, stadi za kazi na uzalendo baada ya hapo wenye sifa za kuajiriwa hupata ajira katika taasisi mbalimbali za serikari na binafsi.
Taarifa hii Imetolewa na Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa.

Wednesday, May 4, 2016

Dar es Salaam yapinduliwa juu chini.

                                                           Maeneo ya Tabata yalivyokua

Mvua zilizonyesha mfululizo katika jiji la Dar es salaam zimeleta maafa makubwa sana kwa wananchi waishio Dar es salaam pia zimeathiri sana Vipato vya walio wengi kwa kushindwa kuendelea na shughuli zao za kila siku baada ya maeneo yao ya kazi kujaa maji.
                                          Biashara za wananchi wa kawaida pia zilisimama

                           Adha ya Mvua pia iliwatesa sana wananchi walio wengi




Tuesday, April 26, 2016

Maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano, Wafungwa waneemeka.





Rais Dk.John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa wote kwa kuwapunguzia 1/6 ya vifungo vyao huku wafungwa 3,551 wakifaidika na msamaha huu baada ya kupunguziwa 1/6 ambao kati yao 580 watachiliwa huru na 2,971 wanabaki gerezani wakitumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 42 ya muungano kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1)(d) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao utawahusu wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya ukimwi, kifua kikuu, na kansa ambao wako kwenye hatua za mwisho, wafungwa waliothibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa mkoa au wilaya.
Wengine ni wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao umri huo umethibishwa na jopo la waganga, wafungwa wakike walioingia na mimba gerezani na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya pamoja na wenye ulemavu wa mwili na akili ambao pia wamethibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa mkoa au wilaya.
Msamaha huo hautawahusu waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa ama kifungo cha maisha, makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya,uombaji na upokeaji rushwa, unyang’anyi kwa kutumia silaha, makosa ya kupatikana na silaha, risasi na milipuko isiyo halali.
Wengine ni wale wanaokabiliwa na makosa ya shambulio la aibu, ubakaji, kunajisi na kulawiti, wenye makosa ya kuwapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliotenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka 18 na kuendelea, wizi wa magari, pikipiki, wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao, waliowahi kupunguziwa kifungo na msamaha wa rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
Waliohukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, biashara ya binadamu, kukutwa na viungo vya binadamu pamoja na vitendo vya mashambulizi na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, usafirishaji wa nyara za serikali na ujangili,wizi/ubadhilifu wa fedha za serikali, kujaribu kutoroka wakiwa chini ya ulizi halali na wale walioingia gerezani baada ya tarehe 26/02/2016.

TCRA YAPATIKANA









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.
Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.
“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua  dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson MsigwaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULUDar es salaam

Friday, April 15, 2016

Sudani kusini yajiunga rasmi JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI




Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametia saini mkataba wa nchi yake kujiunga rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Kiir ametia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita.

Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo baadaye.

Baada ya kujiunga rasmi leo, Sudan Kusini inatarajiwa kufungua mipaka yake kwa ajili ya biashara. Tayari kampuni na asasi nyingi za kifedha kutoka Kenya zimefungua biashara nchini Sudan Kusini.

Wengi wanatarajia hatua ya leo itafungua fursa zaidi za kibiashara kati ya Sudan Kusini na nchi wanachama wa jumuiya.

Wadadisi wengine wanaamini kuwa baadhi ya miradi ambayo Sudan Kusini ingetaka kujumuishwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miundo msingi ikiwemo reli na mabomba ya mafuta.

[​IMG]

Monday, April 11, 2016

Sababu zilizoondoa Ukuu wa Mkoa wa Anne Kilango Malecela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa huo Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.
Anne Kilango Malecela
Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo April 11 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.
Rais Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana Aprili, 10 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.
Pamoja na hatua hiyo, Rais Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Katikati ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.
Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.

Breaking News: Rais wa Zanzibar Dr Shein atangaza rasmi kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM.









Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa isipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

Diamond Amaliza ziara ya Ulaya, Adai Reality TV Show yake itaweka Wazi Mambo Mazito

Diamond Platnumz amemaliza ziara yake ya Ulaya aliyoipa jina, From Tandale to The World Tour iliyompeleka kwenye nchi takriban nane.

Show yake ya mwisho ilifanyika Jumamosi hii jijini Copenhagen, Denmark ambayo video zake inaonesha ilikuwa na mafanikio makubwa.

Mchumba wake Zari aliyemsindikiza kwenye nchi zote alizopita, ameshukuru kwa kuandika: Allow me to thank everyone that helped us while out there in Europe. For showing us around and hosting us. Mostly thank you for allowing my hubby entertain you. Stay blessed.

Tayari Zari amerejea Afrika Kusini kuungana na familia yake.

































Katika hatua nyingine Diamond amedai kuwa reality TV show yake ijayo itaweka wazi mambo mengi mazito.

“Can you try to guess the name of our Reality Show?) (Muda si Mwingi Kipindi cha Maisha yangu ya kila siku, Familia na Team yangu nzima itaanza kuwa kwa Tv yako pendwa, ” ameandika Instagram.

“Nakuahidi sio tu eti Kireality show … ni Reality show Bora ambayo naamini utaipenda kunzia kwenye Quality, Mikasa na matukio yote nnayopitia mimi, Familia na Team yangu kila siku….Mengi yanaonekana, Unayoyasikia, Unayasoma ila kwenye Hiki kipindi ndio itakuwa Thibitisho la kila uvumi uusikiao….Sjui Kipini puani, Mara jicho, Mara sjui @officialshetta , Mara DNA, Mara @romyjons kutoinekana tena kwenye Tour Ghafla….Niamini mimi yote utaona na kuyapata kwa uwazi kabisa, Kaa na Mimi…….! We unavyohisi reality Show yetu itakuwa inaitwaje…..?” ameongeza.

UFUSKA WA MASTAA BONGO







Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja NI laana! Baadhi ya mastaa wamenaswa laivu wakifanya vitendo vilivyotafsiriwa kuwa vya kifuska, Ijumaa Wikienda lina mkanda kamili. Baadhi ya mastaa wakionyeshana ufundi wa kucheza. Tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya Victoria, Dar wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto wa mjini, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’.…
GPL 

TABIA YA LULU KERO BONGO MUVI







Stori: Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata 
WAMEANZA! Tabia ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kutojumuika na wenzake kwenye matukio ya kijamii hasa matatizo inadaiwa kuwakera Klabu ya Bongo Movie Unity hivyo kuandaa kikao maalum cha kumkanya. Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’. Habari kutoka kwa chanzo chetu makini, zilidai kwamba malalamiko hayo ya kuwa Lulu amekuwa mzito kuhudhuria shughuli za wenziye kama misiba au hata sherehe zilianz

KITUMBUA Kimeingia Mchanga...Ikulu Yafuta Safari ya Wakuu wa Wilaya 10 Kwenda China China







Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi

Ikulu imefuta safari ya wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi idadi kama hiyo waliotakiwa kwenda China kwa mafunzo ya uchumi wa kimaeneo kuanzia jana, na kuna uwezekano mkubwa ikatangaza uteuzi mpya leo.

Wakuu hao wa wilaya na wakurugenzi wao  walikuwa waondoke jana kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, lakini habari zinaarifu kuwa Ikulu iliamua kutotoa kibali, hali inayozidisha ubashiri kuwa uamuzi huo umetokana na kukamilika kwa uteuzi wa wakuu wapya.

Safari hiyo ilishakamilika kwa kiwango kikubwa baada ya kupata visa na wengi wao kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa safari hiyo, lakini wakalazimika kurejea kwenye vituo vyao baada ya kukosa kibali cha Ikulu ambacho hutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi.

Mara tu baada ya kuapishwa Novemba 5 mwaka jana, Rais John Magufuli alitangaza kudhibiti safari za nje za watumishi na viongozi wa umma kwa kuagiza kuwa Ikulu ndiyo itakayotoa kibali baada ya kujiridhisha na umuhimu wa safari hizo kwa Taifa.

Tangu atoe agizo hilo, ni mawaziri wawili tu ambao wameruhusiwa kwenda Vietnam kwenda kujifunza kilimo na viwanda. Mawaziri hao ni Mwigulu Nchemba (Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi) na Charles Mwijage (Viwanda na Biashara).

Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji alikwenda nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa fedha, wakati kwa nyakati tofauti Makamu wa Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikwenda Afrika Kusini na Botswana.

Mpaka sasa, Rais Magufuli amefanya safari moja tu ya nje alipokwenda Rwanda kwenye maadhimisho ya mauaji ya kimbari.

Lakini safari ya wakuu hao wa wilaya ilikuwa ifadhiliwe na China, kwa mujibu wa habari hizo na hivyo isingeisababishia Serikali kutumia vibaya fedha za walipa kodi.

Uamuzi huo unaonekana kuzingatia zaidi uteuzi wa wakuu wapya ambao taarifa zinasema unaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, wakati wa wakurugenzi wa wilaya unatazamiwa kutangazwa baadaye wiki hii au wiki ijayo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alikiri kuwapo kwa safari hiyo, lakini akasema hajui kama imeidhinishwa na Ikulu kwa kuwa si muhusika.

“Katika hatua za awali nilisaini safari hiyo kuwaruhusu waende China, lakini sijui kama wamenyimwa kibali kwa sababu hilo si suala la ofisi yangu,” alisema Waziri Simbachawene.

Kama ni kweli, alifafanua Simbachawene, inaweza kuwa ni kutokana na umuhimu wao wa kuwatumikia wananchi kwenye maeneo wanayotoka. “Hawawezi kuondoka na kuziacha wilaya zao ilhali wao ndiyo waangalizi,” alisema Simbachawene.

Akiwa Chato mkoani Geita, Rais aliwataka wakuu wa wilaya kuchapa kazi badala ya kuwa na woga wa kutoteuliwa akisema uchapaji kazi ndio utawafanya waendelee kuwapo kwenye nafasi zao.

Rais pia amekuwa akitoa maelezo kadhaa yanayoonyesha atafanya uteuzi kwa kutumia vigezo hivyo, hasa suala la elimu ambayo inakabiwa na tatizo kubwa la uhaba wa madawati na vyumba na majengo, kipindupindu, njaa, migogoro ya ardhi na watumishi hewa.

JIFUNZE NAMNA YA KUENDESHA BIASHARA YAKO HAPA KWA HUYU NDUGU.

KAMA UNA NDOTO YA  # KUJIJIRI  AU KUFANYA  # BIASHARA  USIOGOPE ILA JIFUNZE KIDOGO HAPA! Naitwa Andrea. Na nakutana na watu we...