Wednesday, February 7, 2018

DALILI ZA HATARI KWA MTOTO WAKO

zijue dalili hizi za hatari kwa mtoto wako

Mtoto mwenye dalili mojawapo zifuatazo anahitaji matibabu haraka na uangalizi wakati wote. Akipatiwa huduma, anaweza taratibu kupata nafuu. Kama ana dalili zifuatazo zaidi ya moja, au iwapo dalili yoyote itazidi kuwa mbaya, mtoto yu hatarini:
  • Kupungukiwa na maji mwilini. Kukosa mkojo, mdomo kukauka, au utosi kwenye kichwa cha mtoto kubonyea ndani ni dalili za kupungukiwa na maji mwilini-tatizo linalotishia uhai wa mtoto. Angalia chini -sehemu ya kupungukiwa na maji.
  • Mashambulio ya ghafla kwa mtoto ambayo hujumuisha kupoteza fahamu na kurusha maungo ya mwili au kutetemeka- kawaida huambatana na homa kali.
  • Ulegevu mwilini. Udhaifu na uchovu wa mara kwa mara mwilini siyo hali ya kawaida na wala dalili ya afya nzuri. Kukosa hamu ya kula na kuchanganyikiwa kimawazo hasa ni dalili zinazoibua wasiwasi. Kuugua sana ugonjwa wowote ule huweza kusababisha tatizo hili.
  • Kupumua kwa shida au kupumua haraka haraka. Hizi ni dalili za kichomi au nimonia  ugonjwa ambao ni hatari sana kwa watoto wadogo.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE NAMNA YA KUENDESHA BIASHARA YAKO HAPA KWA HUYU NDUGU.

KAMA UNA NDOTO YA  # KUJIJIRI  AU KUFANYA  # BIASHARA  USIOGOPE ILA JIFUNZE KIDOGO HAPA! Naitwa Andrea. Na nakutana na watu we...